23

MBIO ZA KUJIFURAHISHA KKKT USHARIKA WA AMBURENI

“KIJANA KIMBILIA KWA YESU”

“KIJANA KIMBILIA KWA YESU”

“JINSI GANI KIJANA AISAFISHE NJIA YAKE? KWA KUTII,AKILIFUATA NENO LAKO” ZABURI 119:9

Msaidizi wa Askofu Mch.Ndelekwa K.Pallangyo akiwa mgeni rasmi katika kongamano la mbio za kujifurahisha na michezo mingine ya vijana yaliyoandaliwa na Usharika wa Ambureni KKKT Dayosisi ya Meru tarehe 26.06.2021.

Akifungua mashindano hayo mchungaji kiongozi wa Usharika wa Ambureni Mch.Exaud Aminiel Nnko alisema mashindano hayo yenye kauli mbiu “”KIJANA KIMBILIA KWA YESU” yameandaliwa na idara ya vijana yakiwa na lengo la kuimarisha vijana KIROHO NA KIAFYA na kuwahamasisha vijana kuja kanisani badala ya kukaa vijiweni na kujihusisha na matendo maovu.Amesema mashindano hayo yameandaliwa na idara ya vijana usharikani hapo.Mbali na vijana pia walishiriki watu wa rika tofauti tofauti.

Mbio hizo zilikuwa za umbali tofauti yaani.

 • Mbio za kilomita kumi (10).
 • Mbio za kilomita tano (5).
 • Mbio za mita mia moja (100).

Akisoma risala katika mbio hizo za kujifurahisha ndugu Abel Ngira amesema mbio hizo zimelenga kumrejesha kijana wa Kristo,kujitambua thamani yake na wajibuwake kama kijana,jamii na hata taifa.Ametaja changamoto mbali mbali zinazowakabili vijana kuwa ni pamoja na mitaji pamoja na vijana wengi kutohudhuria kanisani.Amesema ili kukabiliana na achangamoto hizo Vijana Usharikani hapo wameanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki wadogo na hadi sasa wamefikisha mizinga mitano na malengo ni kufikia mizinga 100 ifikapo mwaka 2025

Naye mratibu wa mbio hizo Usharikani hapo Irene Kimaro amesema mbio hizo zimelenga kumrejeza kijana kwa Yesu kwa kuweza kujitambua kiroho,kiakili na kiafya kupitia mazoezi.

Akiongea na vijana wa Ambureni Mtumishi Erick K.Urioh amesema KILA KIZURI HUTOKA KATIKA KICHUNGU aliwaasa vijana na kuwaambia kuwa kila jambo zuri linatokana kazi ngumu iliyofanyika kabla,akitoa mfano ili upate madini mazuri ya Tanzanite lazima mtu achimbe na kutokwa jasho sana. Aliwashauri vijana kufanya kazi kwa uaminifu na kumcha Mungu maana kijana mcha Mungu ndiye hufanikiwa na ndiye anayependwa na kutegemewa na kanisa na taifa.

Akihutubia vijana wa Ambureni na kutoa neno la shukrani Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Meru Mchungaji Ndelekwa K.Pallangyo amewaasa vijana kutumia nguvu zao kwa kufanya kazi kwa kujituma na kulitumikia kanisa. Amesema vijana wengi wanatumia nguvu na muda wao vibaya kwa kufanya matendo maovu na kukaa vijiweni badala ya kwenda kanisani. Amepongeza Mchungaji kiongozi,Idara ya vijana na viongozi wote wa Usharika kwa kuandaa mbio hizo za kujifurahisha kwani zimewaleta vijana pamoja na kuwaomba waendelee na moyo huo huo na kuhakikisha vijana wanamjua Yesu Kristo pamoja na kulitumikia Kanisa na Taifa kama kauli mbiu yam bio hizo inavyosema “KIJANA KIMBILIA KWA YESU” .Amewakabidhi washindi mbali mbali zawadi na medani washiriki wa mbio hizo za kujifurahisha.Mbali na mbio za kujifurahisha Msaidizi wa Askofu amezindua timu ya Mpira wa miguu usharikani hapo na kukabidhi vifaa kama mipira n.k

Kwenye tukio hilo vijana 37 waliokoka na kumpokea Yesu Kristo kama Bwaana na Mwokozi wa maisha yao akiwepo mshindi aliyeshika namba mbili mbio ndefu za kilomita kumi.

Mbio hizo za kujifurahisha zilidhaminiwa na wadhamini mbali mbali wakiwepo 

 • Duluti Kahawa Garden.
 • Highland hardware.
 • Nano Electric Works
 • GMX Holding ltd.
 • Elite atorneys
 • Pina Secretarial
 • GEM 2010 Electrical Supply
 • RIL Solution
 • Eseh Investment
 • BEGOTI Enterprises.
 • Simon Safaris
 • Maji ya Shafi
 • Coca Cola.

 

Makala hii Imeandaliwa na Barakaeli Aremu Nnko 0765/0785 991637