Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Meru (KKKT DME) ni miongoni mwa Dayosisi 26 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Dayosisi hii ilizaliwa rasmi tarehe 21 Juni 1992 na kupata cheti cha Usajili no. SO. 7724 tarehe 16 Julai 1992.

Dayosisi hii awali ilikuwa ni Jimbo chini ya Dayosisi ya Kaskazini na imepakana na Dayosisi ya Kaskazini Kati kwa upande wa Magharibi na Kusini pamoja na Dayosisi Kaskazini kwa upande wa Mashariki na upande wa Kaskazini ni Mlima Meru. Dayosisi ya Meru huudumia kwa sehemu kubwa eneo lililopo Jimbo la Uchaguzi la Arumeru Mashariki lenye eneo la Kilometa za mraba 1,483. Wakazi wengi wa eneo hili ni Wakulima na Wafugaji.

Majimbo, Sharika na Vituo Dayosisi ya Meru kwa sasa ina Majimbo 5 ambayo ni; Jimbo la Kati, Kusini, Magharibi, Mashariki na Kaskazini. Jumla ya Sharika ni 59 na mitaa ipatayo 166. Idadi ya Wakristo kwa sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya 80,000.

Katika kuhubiri Injili ya Yesu kwa matendo Dayosisi ya Meru inaendesha vituo vya Elimu na huduma za afya. Kwa sasa inasimamia shule za Sekondari 8, Sekondari ya Ufundi 1, Vyuo vya Ufundi 2, Shule ya awali na msingi ya mchepuo wa Kiingereza 1, Hospitali 1, Kituo cha Afya 1 na Zahanati 2.


Our Staff

Elias Nasari

Askofu

Ndalekwa Pallagyo

Msaidizi wa Askofu

Lazaro Urio

Katibu Mkuu

Elisante Maturo

Mtunza Hazina

Godwin Pallagyo

Afisa Rasilimali Watu