23

Utengenezaji wa Sabuni

Katika kuwalea wananchi wa Meru Kimwili na Kiroho Mradi wa Afya na Maendeleo uliopo chini ya KKKT Dayosisi ya Meru unatoa mafunzo mbalimbali ikiwa nia pamoja na Ujasiriamali ili kuongeza kipato kwa jamii. Hawa ni baadhi ya wawakilishi wa Vikundi (VICOBA) ambavyo vimepatiwa mafunzo ya Utengenezaji wa sabuni za maji na za kipande ili kuongeza kipato cha Kaya.Mafunzo haya yaliwawezesha wanufaika kujifunza njia,mahitaji ya utengenezaji wa sabuni ya kipande,sabuni ya  maji,sabuni ya Unga pamoja ya mafuta ya maji (Lotion). Mbali na kujipatia kipato utengenezaji wa sabuni ni msaada mkubwa kwa jamii kwani wanaweza kuzipata kwa urahisi na kwa bei nafuu na kupunguza ukali wa maisha.